Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari Absalom Kibanda amerejea leo nchini baada ya kupata matibabu yake nchini Afrika Kusini ambako alipelekwa baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana tangu mwezi wa tatu mwaka huu, Absalom Kibanda amepokelewa na wahariri, Waandishi wa habari na watu mbalimbali kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere ambapo aliwasili ndege ya kwa shirika la ndege la Afrika Kusini SA, Crew ya Fullshangwe inakupa pole lakini pia tunaomba mungu akupe nguvu na ujasiri zaidi kwani wewe ni mja wakeTuesday, 4 June 2013
ABSALOM KIBANDA AREJEA TOKA KWENYE MATIBABU SA
Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari Absalom Kibanda amerejea leo nchini baada ya kupata matibabu yake nchini Afrika Kusini ambako alipelekwa baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana tangu mwezi wa tatu mwaka huu, Absalom Kibanda amepokelewa na wahariri, Waandishi wa habari na watu mbalimbali kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere ambapo aliwasili ndege ya kwa shirika la ndege la Afrika Kusini SA, Crew ya Fullshangwe inakupa pole lakini pia tunaomba mungu akupe nguvu na ujasiri zaidi kwani wewe ni mja wake| Reactions: |
MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA WAWASILI NCHINI TAYARI KWA MAZISHI
Waombolezaji wakibeba mwili wa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Marehemu Albert Mangwea aka Ngwair wakati alipowasili leo alasiri kwenye uwanjua wa ndege wa Mawlimu JK Nyerere kwa ndege ya shirika la ndege la South Africa Airways kutoka nchini Africa Kusini alikokuwa akiishi, Albert Mangwea alifariki hivi karibuni nchini humo ambapo habari zisizo rasmi inadaiwa zinadai alikula chakula chenye sumu.
Umati wa waombolezaji ukijaribu kulikaribia jeneza la msanii huyo huku watu wngine wakijaribu kupiga picha wakati mwili wake ulipowasili kwenye uwanja wa JK Nyerere leo. | Reactions: |
Monday, 20 May 2013
Thursday, 9 May 2013
RAIS KIKWETE AIAGA BATALIONI ITAYOJIUNGA NA MAJESHI YA UMOJA WA MATAIFA YA KULINDA AMANI DRC
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia. | Reactions: |
WABUNGE WATAKA UMOJA KULINDA AMANI, WACHOCHEZI KUDHIBITIWA
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO, DODOMA
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeazimia kuitaka Serikali kuchukua mara moja dhidi ya viashara vya aina yoyote ya uvunjifu wa amani unaojitokeza ilikuwapa wananchi matumaini ya kujumuika na kubudu kwa uhuru bila kuwa na hofu ya usalama wao.
Azimio hilo limepitishwa leo Bungeni kufuatia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah alipowasilisha Azimio la Bunge la Kulaani Tukio la Kulipuliwa kwa Bomu katika Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti, jijini Arusha , Mei 5,mwaka huu.
| Reactions: |
Wednesday, 8 May 2013
CHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU
Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;
| Reactions: |
MH. PINDA AWAFARIJI WALIOJERUHIWA KWENYE TUKIO LA BOMU JIJINI ARUSHA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya majeruhi wa bomu la kutupwa kwa mkono lililolipuka katika kanisa Katoliki la Olasiti Arusha wakati alipowatembelea kwenye hospitali ya mkoa wa wa Arusha, Mount Meru, May 8,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
| Reactions: |
Subscribe to:
Posts (Atom)

